KISWAHILI KITUKUZWE KISIFUKUZWE

Umewahi kujiuliza ni wapi tungekuwa bila ya lugha ya kiswahili? Kama jibu lako ni tungekuwa mbele  basi jua kwamba wewe unakifukuza kiswahili. Kama jibu lako ni tungekuwa nyuma sana basi jua kwamba wewe unakitukuza kiswahili.

Washairi walitunga mashairi kwa kusifia kiswahili na lugha zote kwa ujumla. Malenga Guru Ustadh Wallah Bin Wallah katika diwani yake ya Malenga wa Ziwa Kuu anasema kwamba bila lugha tutakwama.Na ni kweli kabisa. Ni ukweli mtupu kwamba bila lugha tutakwama.

Kutoka kushoto: Jeppe, Msonobari na Chiara. Hao ni baadhi ya wazungu wanafunzi wa Kiswahili katika ofisi kuu za Kampamso, jijini Nairobi-Kenya

Misahafu inarekodi Mungu Akilalama na kusema kwamba, kama binadamu watakataa katakata kumsifu basi Yeye katika Uungu wake Ataamuru mawe kupata uhai na kuanza kumsifu. Kumekuwa na wazawa wasaliti wa kiafrika ambao wamekidunisha sana kiswahili na kukiona kwamba hakifai. Badala yake wakatukuza lugha za wenyewe ambao hata nao hawajivunii lugha hizo tena. Hamna neno ni haki yao kufanya wapendavyo. Kwenu ndugu zangu kufu langu, Shime na Hongera! Washiriki wote wa Kituo cha Lugha cha Kampamso kongole!! Hamna kundi jingine kama ninyi.

Sisi wapenzi na waenzi wa Kiswahili tukishindwa kupata wafrika ngozi nyeusi kutuunga mkono katika kukipigia debe kiswahili hatutatahayuri katu kwani tayari tumepata mawe ambayo tumeyatia uhai na yatatusaidia kusifu  na kukisifia kiswahili. Mawe hayo yanatokea uzunguni kote kule. Wenzetu hao wameamua kuyavulia nguo maji ya kiswahili na hata kuyaoga.  Mimi nimeshika dodoki moja nawasugua kwelikweli kwenye uti wao wa mgongo wa lugha ya kiswahili ili wanyoke twaa kama barabara ya kuenda mbinguni.

Ili wanyoke twaa kama barabara ya kuenda mbinguni.

Wewe nawe unafanya nini? Usipojivunia Kiswahili utajivunia nini? Kikwenu ambacho ukikiweka mbele sana mnachinjana kama wanyama? Kazi kwako yangu naikomelea hapo. Kumbuka Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe.

Unaweza kunipata katika: msonobari@gmail.com au skype:  msonobari

Advertisements

155 Responses to “KISWAHILI KITUKUZWE KISIFUKUZWE”

 1. Mambo mazuri haya! Great piece of writing. Indeed, this is the way to go. Cheers!

  • Karibu tena. Weye ndiwe nashukuru kwa kutafuta muda wako kuyasoma makala hayo na kuweza kutolea maoni hivyo. Asante kwa muda wako na moyo wako mkuu wa kukipigia debe Kiswahili.

 2. Indeed, its our national language,na tunafaa tujivunie. Kiswahili kitukuzwe na tukienzi kiswahili.

  • Nashukuru sana Binti Vayoleti kwa msimamo na maoni yako hayo mazuri. Tunahitaji watu kama wewe kama milioni moja hivi na kiswahili kitanenepa kwa sifa sufufu ambazo kitapewa. Wakati mwema.

 3. Kweli kabisa, hapo mwalimu Msonobari ameweza kupasua mbarika peupe, bila kiswahili, Afrika nzima ingekuwa nyuma kweli, na ni lazima tujivunie lugha ya kiswahili na kuipigia debe, maana yake ndiyo lugha bora na rahisi kote duniani. Hongera Mwalimu, kwa utendakazi wako mzuri wa kurahihisha lugha ya kiswahili, kiswahili na kitukuzwe. Asante sana.

 4. Hongera Kaka! Kazi bora kweli!

 5. Hail Kiswahili and its ardent surrogate mothers like Mwalimu Mkuu Mpasua Msonobari

 6. Hongera kaka Msonobari kwa u mstari mbele kwa kuenzi na kusifu lugha yetu teule.

 7. huo wako ni msimamo thabiti kabisa. kwa kweli wengi wetu tunaogelea katika kidimbwi tu. hatujafika kwenye lindi la uswahili.

 8. Hongera na kongole ndugu Msonobari kwa kukipigia dede Kiswahili!
  Shime ndugu! Kiswahili ni chetu sisi Waafrika. Makosa yanayokikabili mkabala Kiswahili yanatokana na sisi wenyewe. Kikiharibika ni sisi ndisi tunaokiharibu. Tujivunie lugha hii kabla ya kuvamia lugha za wengine na kujidai kuwa tuna uhusiano nazo. Mwacha mila ni mtumwa!

 9. nafurahi sasa kuwa kiswahili kikiwa ICU Kenya kina dalili ya kupona na hivyo hakitazikwa Uganda

 10. Bila shaka kiswahili hakipaswi kufukuzwa ije mvua jua liwake! Kama waafrika wakweli, yule anayejaribu kukejeli kiswahili anatuudhi sisi kwa hivyo yeye anakuwa si adui tu bali pia mkataa mila. Ndugu Msonobari hongera sana nimetamani kujifunza kiswahili kwa muda mrefu na kufuatia maudhui haya yako naamini nitafika mbali.
  Mimi ni Paulo kutoka Nairobi , bingwa niko radhi kuomba wako msaada.

 11. Ni wazi kama mchana Ndugu Msonobari kwa makala yako. Kwa kweli kiswahili kimeleta faida si haba na kila mmoja wetu anastahili kukiunga mkono kwani nani asiyefahamu kwamba mkataa ya wengi ni mchawi? Heko na kongole kwako mwalimu.

 12. Bingwa twakuvulia kofia. Kazi yako ni bora sana. Ni ombi letu kwamba siku moja utatutembelea huku tuliko ili uweze kutupatia motisha zaidi. Tutaonana majaliwa yake Maulana. Kwaheri.

 13. Shukrani sana kakangu Msonobari ama kweli Kiswahili tutakienzi sisi wenyewe haswa kama wa Afrika wa Mashariki, Sina mengi ila tu na kuomba uendelee vivo hivo.
  David Rono

 14. kiswahili kitukuzwe na kisifukuzwe daima na dawamu, Mwalimu hongera. Mimi ni simon.

 15. Ustadhi Msonobari, ulimwenguni kote wengi ni wazuri, lakini wewe ni bora. STEPHEN

 16. Kiswahili chako ni kizuri. Kwa hivyo tunakusihi uendelee vivo hivo. Ni miye Pampula Eric Mhadhiri wa mojawapo wa taasisi za habari na tchnologia jijini Nairobi.

 17. Mwalimu mchango wako kwa wapenzi wa kiswahili kote nchini Kenya. Injili ya kazi yako nzuri inahubiriwa kote katika tasisi ya habari na teknolojia ya kenya {KIMT}. Twamshukuru Steve, coz kupitia kwake tumekujua. Sally, NRB-KENYA.

 18. Shukrani mwalimu kazi yako ni bora. Twakuomba uendelee vivyo hivyo. Ni mimi wako David Choge mwanafunzi wa uanahabari.

 19. Hongera sana mwalimu, sisi sote twaku tambua kwa ukakamavu wako hususan kukienzi lugha ya Kiswahili, nakuunga mkono kakangu, pongezi

 20. Hongera sana bingwa, sote tuko nyuma yako. Salome, msomi na mpenzi mkubwa wa Kiswahili!

 21. Samani zilizotengenezwa kwa mti wa msonobari hudumu. Kazi yako ndugu Mwalimu Msonobari ni ya kudumu kama tu mti wa msonobari. Mungu akubariki Mwalimu. Nick, mtafiti wa lugha ya Kiswahili na msomaji wa makala yako ya Kiswahili.

 22. Mimi ni mwanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari katika Taasisi ya Habari na Teknologia ya Kenya. Mwalimu kazi yako ni ya kukata na shoka na inavutia. Kiswahili bila shaka kitukuzwe na kisifukuzwe. Kwaheri kwa sasa.

 23. Jambo Mwalimu Msonobari, nashukuru kwa kazi yako nzuri ya kukitukuza kiswahili. Hongera! Vincy.

 24. Kongole Ustaadhi Msonobari kwa kazi yako mufti sana, wengi wetu twahitaji kujua kiswahili kiundani sana na kimantiki na tukiwa na wewe, mambo yatakuwa shwari bila shaka. Kiswahili kitukuzwe.

 25. Mwalimu kazi yako ni bora. Mimi pamoja na wenzangu Franciscar na Vincy Wairimu twaombe utupe siri ya ufanisi wako. SALLY wa KIMT.

 26. Ama kwa hakika, ninayo furaha isiyo na kipimo hasa baada ya kutua katika ukumbi huu wa lugha ya kiswahili. Zipokee shukrani zangu za dhati kwa kujitolea kikamilifu kutuhamasisha kuhusu kifaa hiki muhimu cha mawasiliano.Kwa sasa sina mengi ila ninao wingi wa matumaini kuwa nitajifunza mengi kupitia kwako hasa katika ukumbi huu. Jina langu ni KAKAVINNIE.

 27. Asante sana Msonobari kwa kazi yako. Tumefaidika pakubwa. Mimi ni mwanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari wa taasisi ya KIMT.
  Eunice

 28. Asante Sana ndugu Mpasua kwa kazi yako ya kueneza umuhimu wa lugha ya Kiswahili.
  Hapa Access Kenya Umahiri wako katika hii lugha hutufurahisha sana.

  Mungu Akubariki.

 29. Ustadhi, tajiriba yako ya kiswahili ni nuru ya maisha. Naomba MOLA Akuzidishie maarifa. Makala haya ni mazuri sana. STEPHEN.

 30. Heko kwako mwalimu msonobari. Wengi wanapo wasifu mashujaa wa taifa hili, wapenzi wa lugha ya kiswahili tunakusifu. Kazi yako bora haina mfano. Hongera kaka. STEPHEN.

 31. Bingwa, kwa hata mawe yataimba na kumsifu Bwana ikiwa binadamu wakosa kumsifu. Maneno yenye busara sana kaka. Kila la heri ustadhi. STEPHEN.

 32. Aisee bingwa. Endelea kuwasugua kwa dodoki na hata ikiwezekana utumie jiwe. Wapenzi wa lugha hii tukufu ya kiswahili tuko nyuma yako. STEPHEN mwanafunzi KIMT.

 33. USTADHI, MOLA na akufungulie milango ya heri. Ubunifu wako una mchango mkubwa kwa wana wasomi wa taifa hili. Shukrani za dhati kwa kazi yako. STEPHEN mwanafunzi KIMT.

 34. Mwalimu kazi yako tumeipokea kwa uzuri hususani sisi wanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari. Endelea vivyo hivyo. F.M mwanafunzi KIMT.

 35. Kumbe pia mimi naweza tajiri kwa kujua kiswahili? Ahsante sana kwa kuniibia siri ya ufanisi kiswahili kitukuzwe. Ahsante sana. Emmanuel Spoo.

 36. Shangwe na utukufu ni kwa lugha ya kiswahili. Kukitukuza kiswahili ni ukwasi na kukifukuza kiswahili ni ufukara. Kongole mwalimu. STEPHEN.

 37. Ni bayana kwamba kila mja anatamani kwenda MBINGUNI. Kwa sabubu njia ya mbinguni ni maridadi, ni kweli kuwa ukifahamu lugha hii ya kiswahili, mambo yako yatalainika kama safari ya mbinguni. Maneno ya busara sana haya bingwa. Nashukuru pakubwa. STEPHEN.

 38. Heko fokofoko bingwa. Ujumbe wako umefika na umegonga ndipo. Kiswahili kinastahili. STEPHEN.

 39. Mwalimu shukrani kwa mwongozo wako wa lugha hii ajiri. Kazi yako ni wimbo mtamu kwa masikio ya wengi. MOLA akubariki. STEPHEN, KIMT.

 40. Mwalimu Mpasua Msonobari pasua njia ya ufanisi. Hata BIBILIA husema kuwa MUNGU atafanyika jibu na njia kwa mambo yote. Hongera kaka. Kwaheri. STEPHEN, KIMT.

 41. Ustadhi, ujumbe wako ni JIWE LA MSINGI kwa ujenzi wa taifa. KENYA bila KISWAHILI ni sawa na arusi bila biriani. Kwa hivyo KISWAHILI KINASITAHILI. STEPHEN, KIMT.

 42. GALACHA, msimamo wako ni dhabiti. Kiswahili ndio HAKI, NGAO na MLINZI wa taifa hili. Sote tujifunge vibwebwe kukienzi na kukitukuza kiswahili. Amina. STEPHEN, KIMT.

 43. Kongole bingwa. Kupitia kwa kiswahili Kenya ilijipatia uhuru. Twakushukuru kwa kazi yako. Ahsante. STEPHEN, KIMT.

 44. Mwalimu, kwa kawaida Benki ni shirika lihifadhilo na kukopesha fedha. Wakati benki inapo geuzwa kuwa mkahawa, haya ni malimwengu. Vivyo hivyo lugha hii tukufu imegeuzwa kuwa mtindo wa ‘sheng’ , kwa hivyo wakati benki zinapo wania nafasi bora, pia ni wakati wa KISWAHILI kuwa kinyang’anyironi. Lugha zote ni nzuri lakini KISWAHILI ni lugha bora na muhimu. STEPHEN, KIMT.

 45. Maishani kuna maneno madogo mfano wa; ahsante, pole, tafadhali na nisaidie ambayo ni muhimu lakini yameshinda wengi. Unapo peana pesa kwa mhudumu wa duka ili upate huduma yake kisha utumie neno NISAIDIE, wengi hushangaa sana. Lakini wakati unapo kitukuza kiswahili ni lazima utalazimika kuyatumia maneno yenye ukarimu. Kiswahili ni lugha yenye heshima.

 46. Baadhi ya wachache waliojaliwa kuiona karne ya ishirini na moja ni ukweli kuwa kiswahili si umasikini bali ni utajiri. Kiswahili ni lugha ajiri na arifu. Ni lugha ambayo imesheheni ujuzi, maarifa, ubunifu na tajiriba. Hongera bingwa kwa ukweli wako. MOLA akuondokee shari na akufungulie milango ya heri. KISWAHILI KITUKUZWE, KISIFUKUZWE. Stephen KIMT.

 47. Hongera sana mwalimu kwa
  wazo lako kuwa utaalamu hutokana na juhudi. Guru Ustadhi Wallah Bin Wallah husema kuwa “msomi mzuri huwa na taaluma nzuri.” msomi anayekienzi na kukitukuza kiswahili huwa na msingi imara maishani. Kongole gwiji. KISWAHILI KITUKUZWE, KISIFUKUZWE. Stephen, KIMT.

 48. Ustadhi maneno yako kuwa nyumbani mwa BWANA kuna mavuno lakini wavunaji ni wachache ni ya ukweli sana. Lugha ya kiswahili ni mavuno ambayo yamekosa wavunaji sawia na walaji. Mchango wako kwa kiswahili ni mbolea yenye rotuba nyingi sana. Endelea kupalilia na kunyunyiza maji kisha wapenzi wa kiswahili watafurahia mavuno yako. Kila la heri. KISWAHILI KITUKUZWE, KISIFUKUZWE. Stephen, KIMT.

 49. Mwalimu heko,kazi yako ni kazi
  inayostahili pongezi si haba,Mungu
  aikweze daraja yako iwe juu zaidi

  Nakumiminia pongezi kwa weledi wako
  katika lughw,Maulana aibariki kazi
  ya akili na mikono yako.

  mMnyonge msonge haki yake mpe,
  nakupa hakiyo mwalimu wastahili pongezi
  kazi yako mashallah.

  Kwa lugha unavyoithamini, imepanda daraja
  yako,kwenye uma wasifika(VIP)nafasi
  yako,kwakheri.
  MWANASHA GASEREGO,KIMT

 50. Endeleza juhudi za kuitukuza lugha ya Kiswahili. Kiswahili ni nguzo muhimu katika ujenzi wa taifa. Kiswahili kinastahili. STEPHEN, KIMT.

 51. Ustadhi, mchango wako kwa wanafunzi wa taifa hili huru ni wa kipekee. Duniani tukisema Haleluya, Mbinguni MUNGU na Malaika husema Amina.. KISWAHILI KITUKUZWE, KISIFUKUZWE. STEPHEN, KIMT.

 52. Bila kiswahili tungekuwa wapi? Jibu ni kwamba tungekuwa Misri. Tungekuwa bado utumwani chini ya minyororo ya Wazungu wakoloni. Mnamo mwaka wa 1963, Kenya ilijipatia uhuru kupitia kwa lugha lugha ya Kiswahili. Ni lugha ya taifa. Mwalimu blogu yako imesheheni ukweli mtupe. Kongole bingwa. Yote tisa, kumi ni kuwa; KISWAHILI KITUKUZWE, KISIFUKUZWE. STEPHEN, KIMT.

 53. Kila mara nijiulizapo mahali tungekuwa bila lugha hii tukufu, jibu ni kuwa tungekuwa nyuma sana. Kwa sababu ya kiswahili wengi wanajivunia kuwa wakenya. Kiswahili ni lugha ambayo imezika ukabila katika kaburi la sahau. Lugha ambayo imeimarisha umoja, uraia, pamoja na utaifa. Hiyo ndiyo sababu mimi pamoja na wapenzi waenzi kiswahili tunakuunga mkono kuwa kiswahili kinastahili. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. STEPHEN, KIMT.

 54. Ustadhi heko. Mara kwa mara nikutanapo na Wazungu hata na Wahindi wakiongea lugha ya Kiswahili, bila shaka mimi huzitambua juhudi zako. Ni ukweli mawe yamehaishwa na yanakitukuza Kiswahili. Swali kwa ndugu zangu wapinga Kiswahili ni je, mnayo matumaini ya ufanisi maishani? Lugha ya Kiswahili ni ngome imara katika ujenzi wa taifa. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Kongole bingwa kwa blogu ya ambayo imesheni siri ya ufanisi. Kwangu mwenyewe imenifaa kwa mafao makubwa sana. STEPHEN, KIMT.

 55. Katika kitabu cha Mathayo {11:28}, Mungu anasema kuwa “Njooni kwangu wote msumbukanao na kulemewa mizigo, nami nitawapumzisha.” Amina. Heko ndugu Msonobari kwa blogu hii ya kiswahili. Ujumbe wangu kwa wale walio na ugumu wa lugha hii ya Kiswahili ni “Njooni kwa blogu hii ya kiswahili ya ndugu Msonobari, na mtarahisishiwa.” usanii huu wa ustadhi Msonobari ni kutoka kwa Mungu. Ameongozwa na Mungu kutusaidia. Ahsante sana mwalimu Mpasua Msonobari. Mola akupe maisha marefu. STEPHEN, KIMT.

 56. Kazi yako mwalimu ni nzuri. Endelea vivyo hivyo. Wengi twatamani kujifunza luga hii ngumu sana ya kiswahili. Tafadhali utusaidie. Churchil Dede, mwanafunzi K.I.M.T.

 57. Nitazidi kukushukuru. Blogu yako ni poa kulìko facebook. Usilekeze kamba. Naamini wenzangu watachangia pia. Asante sana. Churchil Dede, mwanafunzi K.I.M.T.

 58. Bingwa kiswahili kitukuzwe. Kisifukuzwe. Karibu sana kwetu shuleni. Twakusubiri. Ng’amua kiswahili. Emmanuel Spoo. mwanafunzi K.I.M.T.

 59. Mwalimu wengi wameisifia kazi yako. Mimi pia nawaunga mkono. Hapa K.I.M.T hatubaki nyuma. Kiswahili kitukuzwe. Tabitha Mukora. Mwanafunzi KIMT. Bye!

 60. Hujambo mwalimu. Asante kwa kazi yako nzuri. Naamini kwamba Mungu atazidi kukuongoza. Jannet Saulo, Mwalimu, Naivash.

 61. kongole bingwa euice kimt

 62. Shukrani bingwa. Ukumbi wako unazidi kutufaidi. Ili kuitwa mzalendo, sharti na lazima uswahili uwe ndani yako. Nawasihi wapenzi wa lugha hii ajiri wajitokeze na waipigie debe. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. STEPHEN MUKANGAI, KIMT.

 63. Titi la mama li tamu hata kama ni la mbwa. Kiswahili ni lugha yetu, hata kama ni ngumu inastahili. Kiswahili ni chetu na iwapo kuna matatizo yanayoikumba, jibu ni sisi wenyewe. Hongera mwalimu kwa kazi yako. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. STEPHEN MUKANGAI, KIMT.

 64. Sawia mtoto mchanga, kiswahili kilizaliwa, kikalelewa na kikakua. Kwa hivyo kiswahili kinastahiji malezi na mapenzi ili kikue. Ahsante ustadhi. STEPHEN MUKANGAI KIMT.

 65. Asante sana mwalimu kwa maneno yako mateule. Kupitia kwa blogu hii, utukufu wa lugha ya kiswahili ume onekana. Kwa wapenzi -waenzi kiswahili ni sharti na lazima tukitukuze. Shukrani.

 66. Ndugu Mpasua Msonobari wewe ni kipenzi cha wengi. Mimi nikiwa mmoja wa wapenzi wa lugha hii ajiri na arifu, nakuvulia kofia. Wewe ni mmoja wa mashujaa tulio nao kwa sasa. Vita vyako dhidi ya wale wanao songoa kiswahili vitafua dafu. Nakupa asilimia mia na moja. Kiswahili kinastahili kutukuzwa, kisifukuzwe. Stephen, KIMT.

 67. “Biashara ni asubuhi, faida kuhesabu ni jioni.” Wasemao husema. Kwa hivyo mwalimu juhudi zako za kukipigia debe kiswahili zitazaa matunda. Faida itahesabiwa na washindi pekee, na bila kiswahili wewe si mshindi tena. Kwa hivyo kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Stephen, KIMT.

 68. Hongera guru kwa juhudi zako za kuikuza lugha ya kiswahili ambayo ni almasi yeu.Navutiwa mnona kazi yako ambayo kwangu naona inastahili pongezi.Mola azidi kukuongezea maarifa ili uzidi kuikuza almasi hii.Sadakta ustadhi.

 69. Ama ma kweli wewe ni wewe wala hamna mwengine ashabirianaye nawe.Tangu niku fahamu nimezidi kufurahia kazi yako.Weye umtia fora sana kwenye ulingo hu wa kuikuza lugha ya kiswahili.U STADHI UNASTAHILI KUVULIWA KOFIA KWANI WACHACHE MNO WALO NA MOYO ULO NAO WA KUKIINUA KISWAHILI.WEWE NI KIPENZI CHA WENGI.

 70. Wasemao husema wavumapo Papa baharini kumbe wapo wengi,walipoondoka wafalme wa lugha kina mwalimu Hassan bega,shaaban tulidhani hatutapata wengine watakao iendeleza lugha ya kiswahili.Shukrani leo tumewapata kina Pasua Msonobari.Heko kwa kazi yako swafi. MOLA AKUMIMINIZIE MENGI MAARIFA UZIDI
  KUTUJUZA. NDIMI KIPENZI CHAKO.

 71. Ustadhi Msonobari, kazi yako ni sinema ya kupendeza ajabu. Inavutia hata vipofu. Siri ya ufanisi wa lugha hii tajiri ni hii blogu. Kwaniaba ya wapenzi wa kiswahili nasema shukrani. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Stephen Mukangai, KIMT.

 72. Bingwa, mbinu ya kalamu yako ni bora. Hoja zako zimeratibiwa kwa ufasaha. Uzoefu, ujuzi, na tajiriba yako zimejitokeza katika kazi zako. Hongera mwalimu. Stephen Mukangai, KIMT.

 73. Ustadh,zangu ni shukrani kwa kazi maridhawa.Mie na vutiwa mno kwa ukuzaji wako wa kiswahili,licha ya nchi hi kuwa na wasomi wengi wa kiswahili wewe ni mojawapo tu wa wale ambao wamejitokeza kukiinua kiswahili hadi kileleni.Natamani sana siku moja ntakapo kutana nawe aghalabu univuvie sehemu ya ubingwa wako wa kiswahili.Ndimi wako Douglas kutoka papa hapa jijini Nairobi mtaa ni wa Eastleigh.Shukran jitan.

 74. Aisifuye mvua imemunyea. Ustadhi, blogu yako ni asali. Kila kuchao naimarika kwa sababu ya juhudi zako za kukitukuza kiswahili. Kwa ujumbe wako ambao ni ukweli kama mchana wa jua ni kuwa kiswahili kinastahili. Hongera bingwa. STEPHEN, KIMT.

 75. Kiswahili kinastahili. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Biblia inasema mwenye jicho na atazame nami nasema mwenye sikio na asikie. Kongole bingwa. Stephen Mukangai, KIMT.

 76. Shukrani ustadhi. Kiswahili ni nuru ya ustawi. Kenya kama taifa, ustawi wa miundo msingi ikewemo sekta ya elimu na uchumi kwa ujumla inategemea na lugha ya taifa ambayo ni kiswahili. Kongole bingwa. Stephen Mukangai, KIMT.

 77. kiswahili kitukuzwe wala kisifukuzwe.hongera kwa kazi mufti unayo tufanyia.wewe ni ngangari nasi ni ngunguri wa kiswahili.Afrika tukienzi kiswahili kwani ni yetu almasi.

 78. Kiswahili kitukuzwe kwa sababu ni lugha ya Kenya. Pia tunaitumia shuleni, makanisani na hata sokoni kwa mazungumzo. Mimi ni sherry Ahendera mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi ya Kabuku-Limuru. Shukrani.

 79. Kiswahili huninyima usingizi lakini ndo nimegundua jibu. Makala haya ni daktari yangu. Nitawaimiza na wenzangu kuyasoma. Mimi ni Carolyne Iramwenya. Mwanafunzi shule ya upili Gishuru high school-limuru.

 80. Kiswahili kinastahili. Nitakitukuza kiswahili siku zote za elimu na taaluma yangu. Mara si moja nimekashifiwa na watumwa kwamba siifahamu lugha rasmi ambayo ni kimombo, lakini siteteleki katu. Nafahamu fika kwamba ni lugha ya taifa. Asante sana ustadhi kwa mwelekeo. Nitasimama nawewe katika juhudi zako za kutukuza kiswahili. KISWAHILI KITUKUZWE, KISIFUKUZWE. STEPHEN MUKANGAI, KIMT.

 81. Wakati nikiwa kanisani huko Limuru, raia mmoja kutoka Korea kule uzunguni alisimamishwa kusalimia waumini alisema “Mungu akubariki na bwana asifiye.” Salamu hizo zilisababisha kicheko. Kwangu mimi nilikuwa na furaha isiyo kifani kwa sababu mzungu huyo alimtukuza Mungu pamoja na lugha ya kiswahili. Ombi langu kwa ndugu zangu ni kwamba wakati wageni wetu kutoka ughaibuni wanajikakamua kujifunza kiswahili, tusiwacheke, bali tuwasaidie kukitukuza kiswahili. Shukrani.

 82. Kutwa yote na hata kucha sitachoka kuihubiri injili ya utukufu wa KISWAHILI. Kiswahili ni chimbuko la mafanikio. Hongera ndugu Msonobari kwa mwongozo wako ambao umesheheni mbinu anuwayi. Pamoja tutakitukuza na kukienzi kiswahili. Shukrani bingwa.

 83. Wakati huu wa dimba la dunia mashabiki wengi wa soka wanajumuika vilabuni na mikahawani ili kushabikia timu zao. Kwangu ni fursa ya kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa kiswahili. Wapenzi na waenzi kiswahili tuwajibike. KISWAHILI KINASTAHILI KUTUKUZWA, KISIFUKUZWE.

 84. Kaka, Kila kuchao ukumbi wako unazidi kuvutia. Unazidi kutujenga. Blogu hii inajaziba yake. Wachache wanayoitambua sasa facebook hawaendi tena. Kila la heri bingwa. KISWAHILI KITUKUZWE, KISIFUKUZWE.

 85. Wakati mmoja niliwahi kumsikiza Guru Ustadh WallH BIN WALLAH AKISEMA HIVI :kiswahil ni utajiri ambao ukiwa nao hamna anye kukupokonya;kweli,almasi yetu ni kiswahil na pole kwa wale wanao sema wanao zingatia lugha za kigeni.Sikuwatakao zinduka kutoka usingizini sie tuta kuwa tume tamba pakubwa.Nchi ipi duniani iliyo endelea kwa lugha ya kigeni?Mwalimu wewe ni bora na mwingine hatuna.

 86. Utukufu wa kiswahili ungalipo. Utukufu wa kiswahili una baraka kemkem. Kiswahili hoe! Hoee!

 87. Ustadhi, nafurahia kuona kwamba blogu yako yazidi kuvutia kila kuchao. Kazi maridadi sana. Kiswahili ni kiungo muhimu sana katika ufanisi wowote ule. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Stephen, KIMT.

 88. Bingwa, nafurahia kuona kwamba blogu yako yazidi kufurahisha kila siku. Kazi maridadi sana. Kiswahili ni kiungo muhimu sana katika ufanisi wowote ule. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Stephen, KIMT.

 89. Aujuao ukwachu wa tunda ni mlaji. Wapenzi, waenzi na wapenzi wa kiswahili pekee ndiyo wanaelewa umuhimu wa lugha hii. Heko kaka Msonobari kwa mwongozo wako kupitia kwa blogu hii ambayo haina badala yake pengine popote pale. Mwalimu sekta pana ya elimu inakutegemea. Kiswahili kitukuzwe kisifukuzwe. STEPHEN, KIMT.

 90. Mwalimu upo? Jina lako limenawiri na kuwanda kote katika nyoyo za wapambe na wapenzi wa lugha ya Kiswahili. Blogu yako ya kiswahili ni asali. Uchanganuzi na mpangilio wa kazi yako ni bora. Shukran. Kiswahili kinastahili. STEPHEN, KIMT.

 91. Safari ya vita dhidi ya sheng unaipigana vyema. Wakati wa kuungana na kushirikiana ni sasa. Wapenzi wa lugha ya kiswahili tuko nyuma yako. Kongole bingwa. STEPHEN, KIMT.

 92. mwalimu tunazidi kujifunza mengi kutoka kwako. shukrasni.mimi ni mwanafunzi wa habari wa kimt. bye.

 93. mwalimu bado nayapitia makala yako. sintachoka kamwe. family nsima ya kimt iko nyuma yako. karibu sana. mimi na matha mwanafunzi wa habari kimt.

 94. kaka msonobari vipi? karibu sana k.i.m.t. umenigeuza kutoka David hadi kuwa DAUDI. kiswahili kitukuzwe kisifukuzwe. ama una semaje? David Rono wa k.i.m.t.

 95. Sifa bado ni zako ustadhi. Utukufu wa kiswahili ungali unashuhudiwa kote. Kwa maana hiyo tunasema kuwa kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. STEPHEN, KIMT.

 96. Guru Ustadh Mpasua Msonobari,unajisikiaje unapokuwa kwenye hekaheka zako za kila siku na kuwasikia wazungumzaji wakiibworongabworonga nakuiharibu lugha ya Kiswahili? Kila mwaka kwenye vyuo vyetu kunafuzu mafahala wa lugha ya Kiswahili,swali ni hili,baada ya kozi zao0 wanaenda wapi? Vitabu vyetu vya Kiswahili ni vichache mno tulinganishapo na lugha zingine,shinda ni nini?Hongera Ustadhh.

 97. Je ustadhi upo? Wapenzi na waenzi kiswahili tunakuenzi kama mboni ya jicho. Vilevile blogu yako ya kiswahili tunaiduruzu kama vile wanafunzi waduruzivyo wakati wa mtihani wao wa mwisho. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. STEPHEN, KIMT.

 98. Namna gani ustadhi? Kukupongeza sitachoka. Yako ni elimu bila malipo. Tunazidi kufuruhia juhudi zako za kulinda utaifa. Blogu yako ni rotuba katika ujenzi wa taifa. Ahsante sana galacha. Natakitukuza kiswahili asubuhi, mchana, na hata usiku. Kiswahili kinastahili. STEPHEN, KIMT.

 99. Hewaa! Kiswahili kinastahili kutukuzwa, sio kufukuzwa. Wakristo hukutana makanisani, na waislam Misikitini, wote kwa lengo la kumtukuza Mola. Wapenzi na waenzi kiswahili ambao ni mseto wa Wakristo na Waislam, sote tujumuike kwenye blogu ya Kiswahili ya ndugu Mpasua Msonobari kwa lengo la kukitukuza kiswahili. Tafadhali kiswahili kitukuzwe. STEPHEN, KIMT.

 100. kiswahili kitukuzwe daima.ama kwa hakika ni lugha pekee iliyo na uwezo wa kuwaleta watu tofauti pamoja,bila misingi ya kikabila na pasipo karaha. kakavinnie KIMT.

 101. u hali gani bingwa? ukumbi wako bado hai. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. shukran. Mercy wa kimt

 102. Ni lugha yetu. Lugha ya taifa. Hapana pingamizi. Kwa sababu ya Kiswahili najivunia kuwa mkenya. Shukran bingwa kwa mwangaza wako.

 103. u hali gani bingwa? mapishi yako ya kiswahili twayachangamkia vilivyo. kongole kwa kazi yako kwamba kiswahili kiswahili kitukuzwe na kisifukuzwe.Mercy wa KIMT.

 104. Lugha ya Kiswahili ni nuru ya ufanisi. Hata wazungu wametambua ufanisi wa lugha hii teule, na zaidi ya yote wanakitukuza kwa utukufu wa aina yake. Kongole bingwa kwa elimu yako. Shukran..

 105. Je, wewe wakitukuza Kiswahili? Laweza onekana swali balagha kwa sasa lakini, jibu lake lipo na lina uzito wake. Tafakari hayo. MERCY, MWANAFUNZI KIMT.

 106. Tujivunieni kiswahili kwa maana ni lugha ya taifa. Kiswahili kitukuzwe lakini kisifukuzwe. David Choge, mwanafunzi wa habari, KIMT.

 107. Aisee bingwa. Heko kwa kazi yako nzuri. Blogu yako ni ishara ya uzalendo kwa taifa letu. Kiswahili ni lugha yenye uhimu sana kwa taifa letu tukufu, kwa kinastahili kupewa utukufu wa aina yake. Shukran.

 108. Hongera bingwa kwa ujasiri wako. Kazi yako niyakupigiwa mifano. Tia bidii, kwani sisi sote tuko nyuma yako. Kiswahili kitukuzwe wala kisifukuzwe. MADAM JANNET SAULO, MWALIM.

 109. Nashukuru kwa mawaidha yako bingwa. Mimi kama mwanafunzi wa taaluma hii ya uanahabari nahitaji Kiswahili kwa wingi. Kwa hivyo nitaendelea kukitukuza kiswahili kwa utukufu wote. Tabitha Mukora, KIMT.

 110. Ndiyo hivyo tena. Kiswahili ni lugha ya taifa, ingawa inadharauliwa na wengi waso jua maana. Watakapo jua maana watakitukuza kwa utukufu wa aina yake. Kwa wale waso jua maana ni kwamba ni lugha yenye umaarufu na utajiri. kiswahili kitukuzwe wala kisifukuzwe. SPOO, Mwanafunzi KIMT.

 111. Kiswahili kinastahili. ni ukweli mtupu kwamba ni lugha ya taifa. Kiswahili kitukuzwe na kisitukuzwe. Churchil Dede, KIMT.

 112. Wapenzi na wapambe wa lugha ya kiswahili mpo? Mie mzimnazidi kuchangamkia kiswahili kama lugha ya taifa. Nalala kiswahili, nanywa kiswahili, na zaidi ya yote ni kwamba kiswaqhili ni mstakabali wangu. Na wewe je? Ni wazi kwamba bila kiswahili utengamano haupo! Tuiilinde lugha ya Kiswahili kwa maana ya umoja na uzalendo wa taifa letu tukufu. Pasina vitanga viwili makofi hayawezi kulia. Tushirikiane kuindeleza lugha ya taifa. Buriani..

 113. Wambaje bingwa? Hapa bingwa ni kila mpenzi wa lugha. Kiswahili kinastahili utukufu wa aina yake. Tushirikiane kuikuza lugha ya taifa. Ameni..

 114. Ahlan wa sahlan wanalugha. Aisee mie navutiwa pakubwa na mchango wenu kupitia kwa blogu hii ya Kiswahili ya ndugu Mpasua Msonobari. Kiswahili kitukuzwe na kisifukuzwe. Kongele.

 115. Kazi nzuri kiasi kwamba inashinda elimu ya bure. Tujumuike katika kukitukuza kiswahili.

 116. Mwaka 2007 Kenya kama taifa tulishuhudia umwagikaji wa damu kwa sababu ya kuweka lugha zetu za mama mbele. Laiti tungelitumia lugha ya taifa ambayo ni Kiswahili kwa ufasaha, hatungeshuhudia unyama kama huo. Kiswahili ndio silaha ya pekee dhidi ya ukabila. Hivyo basi tunayo kila sababu ya kukitukuza kiswahili.

 117. Maji ukiyavulia yaoge, na likichomoza liote. Wasemao husema. Juzi kuwekuwa na kura ya maamuzi. Wakenya wa tabaka mbalimbali kwa kauli moja tukakata kauli. “NDIYO”. Kama ni maji tumeyavulia. Tuyaoge. Kama ni jua limechomoza. Tuote. Katiba mpya ina ipa lugha ya Kiswahili nafasi ya kuwa lugha rasmi. Tafadhali nakuombeni kuwa tushirikiane katika kuikuza lugha hii ya taifa. Tafadhali.

 118. Tuungane kupigana vita dhidi ya lugha ya mitaani. Kwa maana hiyo Kiswaqhili kitukuzwe na kisifukuzwe.

 119. Natumai wapenzi wa kiswahilim mpo. kiswahili ni chetu hivyo basi tukitunze.

 120. Mbali na siku za awali lugha ya kiswahili sasa ni lugha rasmi na lugha ya taifa. Sasa wakenya tunachangamoto ya kuichangamkia lugha ya taifa. Heko mwalimu Msonobari kwa kazi aali.

 121. navua yangu kofia na kupa zangu kongole,gwiji na mfinyanzi wa chungu cha lugha,stara na kipenzi cha mwana afrika mashariki lugha ya kiswahili,mie niite Mwalimu Hari Mbuti mzaliwa wa sofi morogoro tanzania-naomba kujongea jamvini kila biwi la kiswahili litapolia lisije likanimwaya gwanda la ugwiji ilhali mie kiziwanda.

 122. Salaam aleikum?

  Juhudi hizi za kuimarisha Kiswahili zizidi. Usichoke kutukuza na kukuza Kiswahili. Utazidi kukumbukwa daima kwa mchango wako kuntu na maridhiwa kwa lugha ya Kiswahili. Mapengo yaliyokuwa yameachwa umejaribu kuyakalafati na kukarabati na sasa Kiswahili ni mufti. U kidedea! Kongole na shime!

  • hongera zaidi ndugu msonobari. tungepata ongezeko la wengine 5 kama wewe itakuwa dhahiri shahiri kwamba maadui wanaokifukuza kiswahili tutaweza kuwapiga mieleka..natukienzi kiswahili daima.

 123. Ninawahongera wanamsonobari.

 124. Kaka ni uketo kubaini kuwa kunao waliojitolea kukihusudu kiswahili kama lugha patanishi,Aisee nakuombea mola akuondolee makuruhu akujaze na ujasiri wa kukitetea kiswahili.kwani kupitia kwenu kitafika mbali kwa mbari zote.Kongole shehe.

 125. Ili lugha ya kiswahili itukuzwe lazima kila mwafrika awe mzalendo na lugha ya kiswahili. Kwa kukomesha ukasumba wa kuongea lugha za kigeni ambazo si asili yetu au lugha zetu.

 126. Hakika kiswahili kimepata nafasi yake….hongera ndugu msonobari kwa kutufahamisha haya….

 127. Hongera kwa makala haya…yamenitia hamasa na ari ya kujifunza mengi kuhusu lugha hii adimu na adhimu.

 128. asante na kongole mwalimu mpasua msonobari kwa wosia huu kwetu kizazi cha kiafrika kweli yapendeza kuezi kilicho chako kama lugha hii ya kiswahili.

 129. aisee kaka Msonobari hongera kwa kazi yako kuntu na aula uifanyayo kwa ajili ya kuwaelimisha hao wazungu wanaojua thamani ya Kiswahili kuliko sisi wazawa wa lugha hii maarufu na babukubwa!

 130. BIBLIA

 131. Bidii hizi zisizimike au zifilisike kiswahili ndiyo lugha mwafaka na yenye adabu miongoni mwa jamii

 132. Lugha hii ya Kiswhili tuimarishe kila siku,namshukuru Msonobari kwa jitihada yake kuhakiki lugha hii imenawiri.Heko kaka na uzidi kiubiri njili ya LUGHA HII MUHIMU.

 133. Jamani hili jukwaa tulitumikishe kikamilifu katikakukienzisha, kukieneza na kukihimilisha Kiswahili. Najivunia hakika hii lugha yetu hapa na ambayo ni dhahabu pekee yenye uweza wa kutushikamanisha wana Afrika mashariki na bara nzima hatimaye. Asilimali hii tusiipukutishe kwenye kizazi chetu hiki, yafaa tuwarithishe wanetu kwa faida kuu ya leo, keshoye na kuzidi.
  Yangu nakuvulia…Lugha hii tuienzi.

 134. Aisee,kwendako hisani hurudi hisani hakurudi nuksani.Kongole nakupa kwa michango yako aali.Ama kweli,kama msomi wa Kiswahili hapa chuoni Kenyatta,hamasa yako imenifaa pakubwa.Anayezaliwa akakosa kuacha alama katika ulingo wa kiswahili,nungunungu anayetambaa kwa kuchora ardhi keshampiku!Wasalaam wapenzi wenzangu wa hino lugha tukufu.

 135. Kongole kaka kwa kazi nzuri unayoifanya ili Kiswahili kitukuke. La ajabu ni ni kuwa twapenda kukuza lugha za watu na zetu zimetushinda.

 136. Kiswahili kitukuzwe daima. Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga bingwa hongera.

 137. Najitolea kwa hali na mali kukipenda,kukienzi,kujivunia na kukitukuza kiswahili bwana Msonobari. Hongera ndugu yangu.

 138. Kongole babu kazi nzuri.Wazindue warejee kiamboni.

  Alhamdulillahi kwa umbo adhimu na ashirafu la kiswahili.Wenye uluwa walilumba”Mwacha mila mtumwa”.Si adabu kumwacha ahaliyo akilalamika ukakimbia kwa mke wa jirani.itakuwa ni zinaa na ni haramu.

  Kiswahili kimezaliwa hapa na kulia hapa kimekomaa na chazidi kukomaa.mbona tusikipe mapenzi ya nyumbani? Mbona twakimbilia kichina,kiingereza,kireno na wake wa wenyewe si tuwakuze wetu?Ashakum si matusi, kama huko si kuzini ni nini?Huo si utumwa yakhe?

  Sijasema tusimpende jirani,hasha nnalokusudia ni kwanza tumpambe wa kweti ndo tupate mke wa pili wa tatu na hata wanne.

  Mie ni mpenzi wa kiswahili na wala si mshenzi nayaenzi mapenzi yetu.Kiswahili kitukuzwe na maadui wacho wafukizwe.

 139. Napenda lugha ya kiswahili lakini ningegenda kujua umuhimu wa kosi ya kiswahili kwa mwanafunzi

 140. Kiswahili kiendelezwe
  na kisi fukuzwe
  nahisi kila mtu anapenda
  hilo.
  Navilevile nko naswali langu ni nchi gani africa inaongea kiswahili faswaha?
  Na ninani mbunifu wa lugha ya kiswahili?

 141. safi sana kwa kukitukuza kiswahili pamoja tuseme kiswahili kitukuzweeee

 142. Hongera sana mwanangu

 143. Ni vyema sana kukarabati Kiswahili na kujivunia lugha ambayo kwayo hamna ubaguzi wa aina yoyote! Jinsi wakenya wanavyojivuni kuwa wakenya, nasi pia tujivunie kuwa Waswahili!

 144. Naomba kufahamishwa umuhimu Wa lugha ya Kiswahili katika Afrika Mashariki

 145. Kongole Kwa kazi sheshe

 146. Mie ni mmoja wa wapenzi wa dhati lugha hii yetu. Ni malenga anayetafuta jukwaa la kughani.Nipe mawaidha.

 147. this is great..lets give kiswahili the first priority

 148. inapendeza ,kiswahili lugha yangu milele

 149. Kongole gwiji na nguli mtetezi wa Kiswahili.Nami naungana na kuungama nawe kuwa Kiswahili kisifiwe na kisifukuzwe au kukashifiwa.

 150. vyema sana nabisha

 151. Kazi Bora kweli kaka Msonobari, Kongole kwa kuwa Balozi mwema wa Lugha ya Kiswahili. Kazi ya Mikono yako ibarikiwe na uenee kotekote ulimwengu.

 152. Kaka Msonobari Hongera Sana kwa Ubalozi wako bora huu wa kueneza lugha ya Kishwahili. Kazi nzuri sana hii. Barikiwa na uenee kotekote ulimwenguni.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s